NIPASHE;BAADA YA KUMTUKANA WAZIRI MKUU,HATIMAYE SUGU AOMBA MSAMAHA - HABARI ZA MPEKUZI BLOG, BOSS NGASSA, RAHATUPU BLOG AND BONGOCLANTZ
Headlines News :
Home » » NIPASHE;BAADA YA KUMTUKANA WAZIRI MKUU,HATIMAYE SUGU AOMBA MSAMAHA

NIPASHE;BAADA YA KUMTUKANA WAZIRI MKUU,HATIMAYE SUGU AOMBA MSAMAHA


Mhe Sugu
Waziri Mkuu, Mhe. Pinda

BAADA ya kauli yake iliyoibua mjadala mkubwa nchini dhidi ya Waziri Mkuu, Mhe. Mizengo Pinda kufuatia majibu yake aliyoyatoa wiki iliyopita Bungeni kwa kutaka Polisi kuendelea kuwapiga raia,
Mbunge wa Mbeya Mjini, Mhe Joseph Mbilinyi 'Sugu', aomba radhi.

Sugu amemuomba radhi mhe Pinda na watanzania kwa ujumla kwa lugha aliyotumia katika kuonyesha hisia zake juu ya kauli aliyoitoa mhe Pinda bungeni.

Kupitia akaunti yake ya Facebook, Mbunge huyo machachari amenukuliwa akiwaomba radhi Watanzania waliokerwa na kauli yake iliyodai kwamba Tanzania haijawahi kuwapata Waziri Mkuu kama Mhe. Pinda kwa kusema;

"Ndugu watanzania, naombeni radhi kwa tusi nililolitoa kwa mhe Pinda, kwani nilikua nimeghafirika, halikuwa kusudio langu kumtukana mmoja wa viongozi wa nchi."
Share this article :

0 comments :

Speak up your mind

Tell us what you're thinking... !

Random Post

ARUSHA
 
Template Design by Creating Website Published by Mas Template