| Lord Eyez (kulia) akiwa na wakili wake wakati wakiongea na waandishi wa habari | 
Mweusi  toka A- City, Lord Eyez amekutana na waandishi wa habari akiwa na  wakili wake ili kuzungumzia kesi inayomkabiri ya wizi wa vifaa vya gari  ambayo ili-make headlines sana siku kadhaa zilizopita.
Lord  eyez amesema yeye kwa sasa anaiachia mahakama ambayo ndiyo itaweza  kuchukua maamuzi ya kisheria kama yeye alihusika ama hakuhusika katika  wizi huo wa vifaa vya gari. 
Wakili  wa msanii huyo anayejulikana kwa jina la Peter Kibatala amesema kesi  hii imefanya mpaka Lord Eyez kuonekana kwamba yeye ndiye mhusika wa wizi  wa vifaa hivyo lakini kwa sasa hivi wanaiachia kwanza mahakama ndiyo  itakayoweza kuchukua uamuzi sahihi kuhusiana na kesi hiyo.
Hizi  kauli za mweusi huyu na wakili wake zinaonekana zimepimwa na ruler ya  kisheria kwa sababu ni kosa kisheria kujadili kesi ambayo iko mahakamani  (commenting on a pending case).
Weusi  nao walisema ‘neno’ kuhusu tuhuma zinazomkabili member huyo na kwamba  tukio hili limewaathili hasa pale wanapokutana na watu mbalimbali na  kusikia story toka kwa watu kwamba wote watakuwa wanahusika katika tukio  hilo wakati ni story ambazo sio za kweli.
Kesi hiyo inatarajiwa kusomwa katika mahakama ya mwanzo jijini Dar es Salaam tarehe 13, 14 na 15 mwezi huu wa Novemba.
Hata  hivyo the N2N soldier amesema kwa sasa anachotaka kufanya ni  kudondonsha ngoma yake mpya kali ambayo anataka kufanya ‘surprise’ kwa  mashabiki wake katika industry ya muziki wa Bongo. 
Lord  eyez alituhumiwa na msanii mwenzake Ommy Dimpoz kuwa alishirikiana na  wenzake kumuibia vifaa vya gari lake na tuhuma hizo nzito ambazo ni pigo  kwa kundi la weusi kiujumla zilipelekea Lord Eyez kukamatwa na  kushikiliwa kwa na jeshi la polisi kwa siku kadhaa na baadae kufunguliwa  kesi mahakamani ambapo alipewa dhamana.
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
0 comments :
Speak up your mind
Tell us what you're thinking... !