Home
                          
                          »
                          
                          » 
                          MAAJABU YA DUNIA; JAMAA AFANYA MAPENZI NA MAMA YAKE MZAZI 
 
MAAJABU YA DUNIA; JAMAA AFANYA MAPENZI NA MAMA YAKE MZAZI 
| Aliyefunga Ndoa na Mama Yake Anena ' Mapenzi Anayonipa Mama Sijawahi Kupata, Msiingilie Mapenzi Yetu' | 
| 
  Bi Condorada Ngonyani akiwa na mumewe ambaye pia ni mwanae wa kumzaa
 | Mama  aliyefunga ndoa na mwanae wa kumzaa wa kiume baada ya mumewe ambaye  ndiye baba wa mtoto huyo kufariki amesema anawashangaa wanadamu  kuingilia mapenzi yao huku mwanae akiwauliza watu mnatutakia nini kwenye  mapenzi yetu? akiongeza kuwa mapenzi anayopata kwa mama yake hajawahi  kuyapata. | 
| Bi  Condorada Ngonyani mwenye umri wa miaka 70 ambaye alifunga ndoa na  mwanae wa kiume ameibuka na kusema anawashangaa watu wanaowasimanga kwa  mapenzi yao moto moto kati yake na mwanae huyo wa kiume Bw. Joseph  Mapunda. 
 Mama huyo na mwanae waliwekwa kitimoto na wanakijiji waliohoji mapenzi  hayo haramu kati ya mama na mwanae. Tukio hilo la kuwaanika hadharani  mama na mwanae liliandaliwa uongozi wa serikali ya mitaa.
 
 Mama Condorada Ngonyani (70) mkazi wa mkoani Ruvuma, aliamua kufunga  ndoa na mtoto wake wa tatu wa kiume wa kumzaa na kisha kuishi naye  kinyumba kama mke na mume.
 
 Wawili hao hawajutii kitendo chao na wameonekana kuona walichofanya ni  sahihi na kuwashangaa wanadamu, majirani zao na jamii kwa ujumla  kuingilia mapenzi yao.
 
 Wananchi wapatao 400, wa mkoa wa Ruvuma walijitokeza kushuhudia  kimbwanga hicho wakati uongozi wa Serikali ya mtaa walipoamua  kuwafuatilia na kuwahoji na kuitisha mkutano wa wanakijiji na kuwaweka  hadharani.
 
 Wananchi wa mkoa wa Ruvuma wameiomba Serikali kupitia Wizara ya Maendelo  ya Jamii, Jinsia na watoto, kufuatilia kwa karibu suala hilo na  kuwaondoa hofu wananchi kama kuna sheria inayomruhusu mtoto na mama  Mzazi kuweza kuishi kindoa.
 
 Alipohojiwa mama huyo, Condorada Ngonyani, alisema kuwa mara tu baada ya  kufariki mume wake, Mzee Mapunda, yeye aliamua kumchagua mtoto wake  huyo Joseph Mapunda, ili amrithi baba yake katika kuumiliki mwili wake  kama ambavyo alikuwa akifanya Baba yake mzazi, ili kuondokana na tamaa  na vishawishi wa kiulimwengu.
 
 Alisema kuwa baada ya uteuzi huo walifunga ndoa ya kimila japo kuna  baadhi ya wanafamilia hawakufurahishwa na tukio ama jambo hilo, lakini  yeye aliamua kufunga masikio na kuamua kuvunja amri ya sita na mtoto  wake huyo wa kumzaa.
 
 Tukio hili ni mara ya kwanza kutokea kwa mkoa wa Ruvuma na hata kwa  Tanzania nzima, ambapo wakazi wa Ruvuma wamekuwa wakibaki na maswali  mengi juu ya tukio hilo na kuhoji jamii sasa inaelekea wapi kwa baadhi  ya Watanzania kuibomoa wenyewe mila na desturi zetu.
 
 Kwa upande wake, Joseph Mapunda, yeye anasema kuwa upendo na mahaba  anayoyapata kutoka kwa mkewe huyo ambaye ni mama yake mzazi, hajawahi  kuupata kokote na kusema kuwa wanapendana sana na wanaheshimiana kama  mke na mume.
 
 Josepha amehoji kulikoni wanadam kuwafuatilia katika mapenzi yao na  kusema kuwa "hawa watu wanaotufuatilia hadi leo hii kutuweka hadharani  namna hii, wanataka nini kwetu?".
 
 Wananchi hao waliofurika kwa Mganga wa Jadi Flora Ndembo, wilaya ya  Namtumbo Mkoani Ruvuma, wameiomba Serikali kuingilia kati suala hilo na  kuchukua hatua kisheria ili iwe fundisho kwa Watanzania wengine wenye  akili kama hizo za kuharibu mila na desturi za kitanzania kirahisi kama  hivyo
 | 
 
 
0 comments :
Speak up your mind
Tell us what you're thinking... !