| Hii ni pikipiki ambayo ni chanzo cha ajali..... | 
Tarehe 10 ya mwezi wa 11 siku ya juma mosi ni moja ya siku ambazo sitozisahau maishani mwangu.
Baada  ya kumaliza majukumu yangu ya kila siku, nilikwenda masaki kumwona  mmoja wa jamaa zangu wa karibu nikiwa na Blogger wangu Bestizzo pamoja  na mwanafamilkia ya wasafi Dumi(Dancer) Mishale  ya saa moja hivi nikiwa maeneo ya masaki karibu na kona ya msasani  nilipata ajali ambayo haikuwa kubwa sana ingawa imesababisha uharibifu  kwa kiasi kikubwa, Kama mjuavyo barabara ya msasani ni ndogo na gari  huwa haziko katika mwendo wa kasi... ghafla dereva wa pikipiki  alikatisha mbele yangu na katika kujaribu kumkwepa nikagonga gari ndogo  aina ya Rav 4 ambapo ilisababisha dereva wa pikipiki kuanguka katikati  ya gari zote mbili. Hiyo ndio hali halisi ya ajali niliyokutana nayo  jumamosi iliyopita.
Namshukuru sana Mwenyezi Mungu kwa kutunusuru wote bila majeraha makubwa zaidi ya maumivu tu ya hapa na pale. 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
0 comments :
Speak up your mind
Tell us what you're thinking... !