JESHI la Polisi Mkoani Tanga limefanikiwa kukamata baadhi ya vitu vilivyoporwa kufuatia ajali iliyosababisha kifo cha msanii wa maigizo na muziki wa kizazi kipya nchini hapa, Hussein Ramadhani Mkiety maarufu kama Sharo Milionea ambaye alikufa baada ya gari aliyokuwa akisafiria kuacha njia na kupinduka.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga, Constantine Massawe amesema kuwa vifaa hivyo vimepatikana kumetokana na jeshi la Polisi kufanya msako mkali kwa kushirikiana na wananchi wa Kijiji cha Songa Maguzoni.
Kamanda Massawe amesema msakohu umefanikiwa kukamatwa kwa vitu hivyo mbalimbali, zikiwemo nguo alizokuwa amevaa marehemu Sharomilionea.
Massawe alivitaja miongoni mwa vitu vilivyokamatwa ni Betri ya gari na Redio ya gari vilikuwa katika gari la marehemuj pamoja na tyrebegi lililokuwa na nguo alizovuliwa marehemu siku ya ajali ambazo inadhaniwa kuwa ndizo alizokuwa amezivaa, ikiwemo sambamba na mkanda,suruali na saa ya mkononi.
Aidha alisema kwamba watuhumiwa walioiba vifaa hivyo walimtumia mtu mmoja ambaye alikwenda kuvisalimisha kwa Mwenyekiti wa Serikali ya Kijiji hicho cha songe, Abdi Zawadi ambapo wengine wanaotuhumiwa kuhusika na wizi huo wakihama kaya zao wamekimbia.
Alisema kuwa Polisi walifanikiwa kuikamata simu hiyo ya mkononi ya marehemu aina ya Blackberry ambayo tayari ilikuwa katika mikono ya mnunuzi na ilishaondolewa chipu kwa lengo la kuuzwa.
“Baada ya kuweka mtego wa kuinunua tumeikuta tayari imeshaondolewa chipu sasa sijui ilikuwa na hela lakini vitu vingine vimesalimishwa kwa Mwenyekiti wa Kijiji “,alisema Kamanda huyo.
Hata hivyo alisema kuwa licha ya watuhumiwa wa wizi huo kufahamika lakini wamekimbia makazi yao tangu kuanza kwa msako huo na kwamba Jeshi la Polisi linaendelea kuwatafuta.
Marehemu Sharo Milionea aliiaga dunia usiku wa kuamkia Novemba 27 mwaka huu majira ya saa 2.00 usiku eneo la Songa-Maguzoni wilayani Muheza mkoani Tanga katika barabara Kuu ya Segera kwenda Tanga baaada ya gari alilokuwa akiendesha kuacha njia na kupinduka.
Sharo Milionea alizikwa Novemba 28 mwaka huu huko Kijijini kwao Lusanga wilaya ya Muheza mkoani Tanga.
credit kwa rockersports
0 comments :
Speak up your mind
Tell us what you're thinking... !