Mwakilishi wa Rwanda katika shundano la Miss East Afrika 2012
Mrembo  atakae iwakilisha Rwanda ni  UMWARI NEEMA (22) ambae ana urefu wa futi  5.9 ambae ni mwanafunzi wa mwaka wa tatu katika chuo cha Kigali Institue  of Education ( KIE) na pia ni mfanyakazi wa Kampuni ya simu za mkononi  ya Tigo jijini Kigali.
Mrembo  atakaeiwakilisha Nchi ya Kenya ni JOAN WAMBUI NDICHO (18) mwenye urefu  wa  futi 5.8 na anayetarajia kujiunga na Chuo kikuu cha Machakos   University College kusomea mambo ya utalii
 Fainali  za mashindano ya Miss East Africa 2012 zitafanjika tarehe 07 mwezi  December mwaka huu katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es salaam  ambapo zitashirikisha Nchi za Tanzania, Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi,  Somalia, Djibouti, Eritrea, Sudan, Ethiopia, Malawi, Madagascar,  Reunion, Comoros, Seychelles, na Mauritius.
 Mashindano  ya Mwaka huu yanayosubiliwa kwa hamu yanatarajiwa kushuhudiwa na  mamilioni ya watu Duniani kupitia kwenye luninga zao na pia kwa njia ya  Internet ambapo yatautangaza utalii wa Tanzania kwa kiasi kikubwa na pia  kujenga umoja wa Afrika mashariki na kudumisha utamaduni wa ukanda huu  wa Afrika.
 Mashindano ya Miss East Africa yanaandaliwa na kumilikiwa na kampuni ya Rena Events Ltd ya jijini Dar es salaam
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
0 comments :
Speak up your mind
Tell us what you're thinking... !