Bremen,Ujerumani.
Katika hali ya utatanishi kiongozi wa Ngoma Africa band kamanda Ras Makunja wa FFU amejikuta  akipewa mashaka ya  maisha na mwanamama moja kisa wimbo "Mama Kimwaga" ! ambao takribani  mwezi mzima wimbo huo na nyingine za bendi zimekuwa zikipigwa mara kwa  mara na kituo cha Radio Funk haus,inayorusha matangazo mjini  Bremen,Ujerumani. Mwanamama moja ambaye aliguswa sana na ujumbe wa  nyimbo hiyo alihamua kutinga katika ukumbi wa mazoezi wa bendi hiyo mjini Oldenburg,mkononi akiwa na bakora ! mdomoni yakiwa yanamtoka maneno ya  hasira,alisikika akidai kuonana na mkuu wa kikosi kazi cha Ngoma Africa  aka FFU kamanda Ras Makunja,kwa bahati mbaya alijibiwa na wanamuziki  walikua pale kuwa Kamanda hayupo,alipoulizwa kulikoni ?Jimama Pesa  huyo alisikika akidai kuwa alikuja kumtia adabu Kamanda Ras makunja wa  FFU,jimama pesa lilikoroma na kutema kibesi kuwa wimbo ule wa "Mama  Kimwaga" ujumbe wake unamnyima raha jimama huyo mwenye kuongea kiswahili  kinachoonyesha kuwa anatoka nchi jirani kwa watani wa jadi. Jimama pesa  hilo limedai kuwa akutegemea kabisa kama wimbo ule wa "Mama Kimwaga"  ungepelekwa tena kwa maDJ wa redio Bremen na kurushwa hewani Ujerumani  kote kwa kupitia sauti ya Funk Haus Europa, wanamuziki aka "maafande"  wa Ngoma Africa band wakimtetea Boss yao Kamanda Ras Makunja,wamedai  kuwa hawezi kuingilia uhuru wa ma Dj wa redio kwa CD hiyo ilikuwapo pale redio siku nyingi,na katika CD hiyo aliyeimbwa ni "Mama Kimwaga"  sasa inakuaje ? kamanda asakwe
na bakora  ka kushtumiwa kuwa anaziwia ridhiki ya mahitaji ya starehe ya jimama pesa .wanamuziki wa ngoma africa
wanamuhoji  mwanamama anayemsaka kwa bakora kamanda wao Ras Makunja,ambaye mara  nyingi anadaiwa kuwa ni mtunzi na mwimbaji mwenye darubini kali. wimbo  huo pia unasikika at www.myspace.com/thengomaafrica pia
 at
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
0 comments :
Speak up your mind
Tell us what you're thinking... !