Gari  aina ya Rav 4 lenye namba za usajili T 770 BNP lililopata ajali eneo la  Tanangozi, Iringa lililokua likiendeshwa na Bw. Ezekiel Mwaiteleke  (Marehemu) majira ya saa sita na nusu mchana na kusababisha vifo vya  watu watano wa familia moja papo hapo jana Desemba 4, mwaka huu.

Gari  aina ya Scania lenye namba za usajili T 840 BST likiwa na tela lake  lenye namba T 566 BNQ likiwa limegongwa kwa nyuma na Toyota Rav 4 huko  Tanangozi, Iringa na kusababisha vifo vya watu watano wa familia moja  papo hapo.
Baadhi  ya akina mama wasamaria wema wa Tanangozi, Iringa wakijaribu  kumpepeleka mmoja ya majeruhi wa ajali iliyotokea jana eneo la  Tanangozi, Iringa likihusisha Toyota Rav 4 T 770 BMP lililoingia nyuma  ya tela lenye namba za usajili T 566 BNQ ambapo watu watano wa familia  moja waliokuwa wakitokea Dar kwenda Mbeya walifariki papo hapo.
Na Francis Godwin, Iringa
AJALI mbaya imetokea mkoani Iringa jana mchana na kusababisha vifo vya watu wanne wa familia moja pamoja na mfanyakazi wa ndani mmoja.
AJALI mbaya imetokea mkoani Iringa jana mchana na kusababisha vifo vya watu wanne wa familia moja pamoja na mfanyakazi wa ndani mmoja.
Ajali  hiyo  imetokea katika  eneo la Tanangozi wilaya ya  Iringa  kwenye kizuizi cha barabara  cha mafundi wa kutengeneza barabara  kuu ya  Iringa -Mafinga  mkoani Iringa mida ya saa nane mchana.
Kwa mujibu  wa mashuda  wa  tukio   hilo  wameueleza  mtandao  wa  www.francisgodwin.blogspot.com   kuwa  chanzo  cha ajali  hiyo ni dereva wa gari dogo aina ya Rav 4   lenye namba  za usajili T 770 BMP kulipalamia lori  lenye tela kwa  nyuma.
Huku  chanzo kikitajwa  kuwa ni kuendesha  kwa mwendo kasi  wa   dereva  wa gari ndogo marehemu Ezekiel Mwaiteleke  na kushindwa   kulimudu na kulipalamia lori kwa nyuma.
Katika ajali  hiyo  abiria  wote  watano akiwemo baba na mama  wa   watoto  wawili  waliokuwemo katika gari  hiyo pamoja na  watoto hao   walikufa papo hapo na maiti  zote  kupelekwa katika Hospitali ya mkoa wa  Iringa.
Majina ya  waliokufa  ni pamoja  na Ezekiel Mwaiteleke ambaye ni  dereva  wa gari hilo na baba  wa familia  hiyo, mkewe Grace Mwaiteleke,  mtoto Kelvin Mwaiteleke (2), Happy Mwandike na mfanyakazi  wao  wa ndani  aliyefahamika kwa jina la Linda Ezekiel  huku majeruhi katika ajali   hiyo ni mmoja na amekimbizwa  Hospital ya mkoa  wa Iringa.
 
0 comments :
Speak up your mind
Tell us what you're thinking... !