Home
                          
                          »
                          
                          » 
                          DJ CHOKA APOROMOSHEWA MATUSI NA WATU WASIOJULIKANA KUHUSIANA NA WIMBO MPYA WA ROMA NA HIKI NDICHO ALICHOKIANDIKA KWENYE FACEBOOK PAGE YAKE!
 
DJ CHOKA APOROMOSHEWA MATUSI NA WATU WASIOJULIKANA KUHUSIANA NA WIMBO MPYA WA ROMA NA HIKI NDICHO ALICHOKIANDIKA KWENYE FACEBOOK PAGE YAKE!

 Naomba  niseme hichi kitu... MIMI NI SHABIKI NAMBA MOJA WA WASANII WOTE  TANZANIA NA KIKUBWA ZAIDI HASWA WALE WANAOFANYA VIZURI KWENYE GAME HILI  LA BONGO. Juzi rafiki yangu na pia patna wangu kwenye business Roma  Tongwe alitoa wimbo wake mpya 2030 na akaamua yeye kuja kivingine yaani  ili uupate wimbo wake lazima uununue kwa shs elfu 3 na hakutaka uwepo  kwenye site au blog zozote. Watu wengi walitarajia wimbo nitauweka  kwenye blog kama nifanyavyo nyimbo za wasanii wengine, sasa sikuweza  kufanya hivyo kutokana sikupewa ruksa na wamiliki wa wimbo huo badala  yake nikawa naupromoti ili watu waweze kuununua kwa namba ambazo ni za  ROMA mwenyewe na si namba zangu. Sasa wametokea watu wamenitukana sana  na kusema wimbo nasikiliza mwenyewe getto na demu wangu bila kufahamu  mimi mwenyewe rafiki mkubwa wa ROMA natakiwa niwe nao ni lazima niununue  ili kumuunga mkono mshkaji wangu ili maisha yaendelee hata nikija na  biashara yangu na yeye pia atanunua ndio urafiki ulivyo. Sasa  nakushangaa wewe unaniita CHOKO kwanza ukiniita Choko naona kama  umekosea herufi badala ya Choka ukaweka O so haliniumi coz nimezoea  kuitwa hivyo na Haters so naona kama unanisifia tu. NATAMKA MANENO HAYA,  NAHESHIMU KAZI YA MTU NA NAHESHIMU JASHO LA MTU NA NDIO MAANA SIWEZI  KUFANYA KITU BILA RUKSA YA MTU, Mtoto mzuri ni yule aliyepata malezi  bora kutoka kwa wazazi wake na akikuwa atanyooka na kuwa vile vile kama  alivyolelewa na wazazi wake. NIMEMALIZA #Roma203  
CLICK HAPA KWENYE ACCOUNT YAKE YA FB DJ CHOKA
  
 
 
0 comments :
Speak up your mind
Tell us what you're thinking... !