Rais  wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania na Amiri Jeshi mkuu Dk.Jakaya  Kikwete akiwasili katika gari maalum la Kijeshi na Mkuu wa majeshi  Jenerali Davis Mwamunyange kwenye uwanja wa uhuru kwa ajili ya   maadhimisho ya miaka 51 Uhuru wa Tanzania Bara 2012 yanayofanyika kila  mwaka Desemba 9, Kauli Mbiu ya Maadhimisho ya Mwaka huu ni “Uwajibikaji,  Uadilifu na Uzalendo ni nguzo ya Maendeleo ya Taifa letu”
Amiri  Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya muungano ya Tanzania Dk. Jakaya  Kikwete akikagua gwaride la vikosi vya Ulinzi na usalaama katika  maadhimisho hayo.
Amiri  Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya muungano ya Tanzania Dk. Jakaya  Kikwete akikagua gwaride la vikosi vya Ulinzi na usalaama katika  maadhimisho hayo
Kikosi cha Brass Band cha majeshi ya Ulinzi na usalama  kikitumbuiza katika maadhimisho hayo
Viongozi mbalimbali wakiwa katika  maadhimisha hayo kutoka kulia ni Rais Joseph Kabila wa Jamhuri ya  Kidemokrasia ya Congo, Mama Maria Nyerere, Rais wa Msumbiji Mh. Armando  Guebuza,Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Dk. Gharib  Bilal na Mzee Ali Hassan Mwinyi rais Mstaafu wa awamu ya pili
Rais  wa Msumbiji Mh. Armando Guebuza akipokewa  na Mkuu wa mkoa wa Dar es  salaam Mh Said Meck Sadik mara baada ya kuwasili kwenye uwanja wa Taifa.
Rais  wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Mh. Joseph Kabila akipokewa  na  Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Mh Said Meck Sadik mara baada ya kuwasili  kwenye uwanja wa Uhuru asubuhi hii.
Mama Maria Nyerere akiwasili kwenye uwanja wa Uhuru kwa ajili ya kuhudhuria maadhimisho ya miaka 51 ya uhuru wa Tanzania.
Waziri  Mkuu wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Mh. Mizengo Pinda akiwasili  kwenye uwanja wa Uhuru kuhudhuria maadhimisho hayo huku akisindikizwa na  Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Mh. Said Meck Sadik.
Mzee Ali Hassan Mwinyi akiwasili kwenye uwanja wa Uhuru kwa ajili ya kuhudhuria maadhimisho hayo.
Vikosi  vya Ulinzi na Usalama vikiwa vimejipanga tayari kwa gwaride  la utii na  heshima mbele ya Amiri jeshi Mkuu na Rais Jamhuri ya muungano ya  Tanzania Dk. Jakaya Kikwete.
Makamu  wa Rais Dk. Gharib Bilal akisalimiana na Mama Fatma Karume mara baada  ya kuwasili uwanjani hapo, katikati ni Waziri Mkuu Mh. Mizengo Pinda.
Rais  Jakaya Kikwete akipokea gwaride la heshima wakati wa maadhimisho ya  miaka 51 ya uhuru wa Tanzania Bara yanayofanyika kwenye uwanja wa Uhuru  jijini Dar es salaam akiwa pamoja na viongozi mbalimbali kutoka nje na  ndani ya nchi
Rais  Dk. Jakaya Kikwete kulia akipokea Gwaride la Heshima lililpokuwa  likipita mbele yake wanaofuatia katika picha ni Rais wa Zanzibar Dk.  Mohamed Shein, Rais wa Namibia Mh. Ifikepunye Pohamba na Mke wa Rais  Mama Salma Kikwete wakiwa katika maadhimisho hayo
Vijana wa chipukizi wakionyesha michezo na ujumbe mbalimbali wakati wa maadhimisho hayo.
Hapa wakionyesha ukakamavu wao huku wakiwa wameshika silaha.
Kikosi  cha wanaanga Jeshi la wananchi JWTZ kikitoa heshima kwa gwaride kali  mbele ya Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jakmhuri ya Muungano ya Tanzania  Dk. Jakaya Kikwete
Kikosi cha ardhini Jeshi la wananchi la Tanzania JWTZ kipita kwa gwaride la heshima mbele ya Rais Dk. Jakaya Kikwete.
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
0 comments :
Speak up your mind
Tell us what you're thinking... !