WAZIRI  wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk. Shukuru Kawambwa leo ametangaza  matokeo ya Mtihani wa Darasa la Saba 2012 uliofanyika nchini kote   tarehe 19 na 20 Septemba, 2012.   
Katika  Mtihani huo Jumla ya wanafunzi 894,881 walisajiliwa kufanya mtihani huo  ambapo   wavulana ni  426,285 sawa na asilimia 47.64  na wasichana ni  468,596  sawa na asilimia 52.36. Aidha, kati ya  wanafunzi hao, wapo  wanafunzi 874,379  ambao walitarajiwa kufanya mtihani huo kwa lugha ya  Kiswahili na wanafunzi 20,502 walitarajiwa kufanya kwa lugha ya  Kiingereza ambayo ndiyo waliyoitumia kujifunzia.  
Wanafunzi  wasioona waliosajiliwa kufanya mtihani ni 92 wakiwemo wavulana 53 na  wasichana 39.  Watahiniwa wenye uono hafifu ambao huhitaji maandishi  makubwa ni 495, kati yao wavulana ni 238 na wasichana ni 257.
 
Mtandao huu utawaletea habari kamili na link ya kupata matokeo hayo wakati wowote kuanzia sasa. 
 
 

 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
0 comments :
Speak up your mind
Tell us what you're thinking... !