


MSANII  wa filamu nchini, Sajuki alidondoka jukwaani juzi wakati akijaribu  kuwasalimia mashabiki wake waliofurika kumtazama kwenye Uwanja wa Sheikh  Amri Abeid, Arusha.
Sajuki   ambaye jina lake halisi ni Juma Said Kilowoko alikuwa akisumbuliwa na  matatizo ya kupungukiwa dawa na kulazimika kwenda kutibiwa nchini India.
Mwingizaji  huyo alipanda jukwaani katika tamasha la lililowahusisha wasanii wa  filamu na muziki, lakini ndoto yake ya kusalimia mashabiki wake  hakuwezekana.
 Mara  baada ya kukabidhiwa kipaza sauti Sajuki alitamka neno moja ”ahhh" na  kudondoka chini na wasanii wenzake walimsaidia kuinuka na kumuondoa  jukwaani hapo.
Akizungumza  na gazeti hili muda mfupi mara baada ya kushuka jukwaani Sajuki alisema  hali yangu si nzuri kwani nahishiwa nguvu na anahitaji matibabu zaidi.
endelea kutembelea ujanatz 
”Kaka hali yangu si nzuri kabisa naumwa, sijisikii vizuri,” alisema Sajuki huku akionekana mnyonge zaidi.
Hata  hivyo, mashabiki wamefurika uwanjani hapo walionyeshwa kustushwa na  hali hiyo na kushutumu wasanii walioamua kumtumia ili wapate fedha ihali  mwenzao ni mgonjwa.
“Hawa  watu wa Bongo movie ni watu wa ajabu huyu mtu anaumwa, badala ya  kumwacha apumzike wenyewe wanamzungusha bila ya kujali afya yake,”  walisema mashabiki hao.
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
0 comments :
Speak up your mind
Tell us what you're thinking... !