Irene Uwoya.
 Kituko hicho kilitokea katika Viwanja vya Leaders Club, Kinondoni  jijini Dar wakati Uwoya alipokuwa akiomba kura mbele ya wasanii wenzake.
Kauli yake hiyo iliwashangaza wengi kwa kuwa Uwoya ni mmoja kati ya wasanii wanaoongoza kwa kuandikwa kwa skendo.
“Hakuna  asiyejua jinsi skendo zilivyonichafua, nilipogundua kuwa zinaniharibia  maisha nikaachana nazo, sasa ole wao wote wenye tabia za aina hiyo,  hakika watanitambua,” alisema na kuzua minong’ono.
Pamoja na minong’ono hiyo, Uwoya alifanikiwa kuwabwaga wapinzani wake Benny Kinyaiya na Lissa Aidan na kuchukua nafasi hiyo.
Nafasi  ya Mwenyekiti ilikwenda kwa Vincent Kigosi ‘Ray’ ambaye hakuwa na  mpinzani na Chick Mchoma ‘Chiki’ alichaguliwa kuwa Katibu.
Simon Mwapagata aliwashinda Juma Chikoka na Chuchu Hans katika nafasi ya katibu msaidizi.
Single  Mtambalike ‘Richie’ hakuwa na mpinzani katika nafasi ya mweka hazina na  Jacqueline Wolper Massawe alimbwaga Cathy Rupia katika nafasi ya mweka  hazina msaidizi.
CREDIT GLOBAL PUBLISHERS 
 
 

 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
0 comments :
Speak up your mind
Tell us what you're thinking... !