| VILIO NA KICHAPO TOKA KWA POLISI VILITAWALA MAANDAMANO YA YA WANAFUNZI WA IFM | 
| Mwanafunzi aliyeshikwa akipandishwa kwenye Difenda. | 
| Utakwenda Tu! | 
BAADA  ya wanafunzi wa Chuo Cha Uongozi wa Fedha (IFM) kwenda kigamboni ambako  Kamanda wa kanda maalum ya Dar es Salaam Suleiman Kova kuwataka  wakawasilishe hoja zao hukohuko ambako wanadai walipeleka majina ya  wahalifu na hayajashughulikiwa, waligoma kufanya mkutano kwenye viwanja  vya mpira eneo la Machava nakutaka mkutano huo ufanyike kwenye kituo cha  polisi Cha Kigamboni ambako wanafunzi wengi wao walielekea huko.
Mara  baada ya kufika kwenye kituo hicho waliamriwa maratatu waondoke waende  kwenye mkutano na Kamanda Kova wakakataa baada ya hapo ndipo mabomu  yakaanza kupigwa. Kwenye mabomu hayo wanafunzi kadhaa walijeruhiwa na  kuumia wengine walipoteza fahamu. 
Hata  hivyo walioshikiliwa wote waliachiwa na kutakiwa kwenda kwenye mkutano  huo ambao uliazimia mambo kadhaa ya utekelezaji ili kutatua tatizo hilo  la wizi kwenye eneo hilo. Kamanda Kova aliwaahidi wanafunzi hao kuwa  watapata mrejesho wa hatua walizochukuwa siku ya tarehe 30 mwezi huu.
 
 

 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
0 comments :
Speak up your mind
Tell us what you're thinking... !