Home
                          
                          »
                          
                          » 
                          DIAMOND THE PLATNUM; SHOW YA DIAMOND PLATNUM @ NEW MAISHA CLUB NI VURUGU TUPU NA CHUPA KUTAWALA KWENYE UKUMBI!
 
DIAMOND THE PLATNUM; SHOW YA DIAMOND PLATNUM @ NEW MAISHA CLUB NI VURUGU TUPU NA CHUPA KUTAWALA KWENYE UKUMBI!
|  | 
| Watu Wakiingia Maisha Jana | 
Jana  Usiku ndani ya maisha club palikuwa na show kubwa ya Usiku Wa Wasafi  ila haikwenda kama ilivyo pangwa na msafi Diamond.Watu waliingia club  hio mapema na tayari kwa show kali kutoka kwa Diamond. Show ilianza saa  saba na nusu na baada ya dakika chache za Diamond kwenye stage fujo  zilianza, Kundi kubwa la vijana wasiojulikana walianzan kutukana watu,  kurusha chupa na viti, kupigana na kupora vitu vya thamani kutoka kwa  mashabiki wa Diamond. Chupa zilipoanza kurushwa kwenye stage ,moja  ilimpata Diamond mkononi na nyingine ilimjeruhi Bestizo Mkononi.Bestizo  ni Camera Men na Social Media Personal Wa Diamond kupitia  Thisisdiamond.com. Diamond alishuka kwenye stage na kwenda kwenye chumba  cha mapumziko mpaka fujo zilipotulizwa.
 
Chid  Benz aliongea na watu na kusema sio kitu kizuri kufanya fujo kwenye  onyesho la msanii kama Diamond.Kwani kama una chuki na Diamond mfate  mtaani na sio kwenye show yake kwani unaweza kuleta matatizo kwa  mashabiki wasio na hatia. Pia Chid Benz alimtuliza Diamond na kumuomba  apande kwenye stage kumaliza show na kuburudisha fans waliolipa na kuja  kumuona mtu wao. 
Vitu  vya thamani kama Cheni,Pete na Camera ya Bestizo ya ThisisDiamond  iliporwa kwenye fujo hizo. Inasemekana Diamond na Uongozi wa maisha  ulipata taarifa kuhusu uwezekano wa fujo hizi kutokea na hatua  zilifanyika kuweka usalama zaidi ila vijana hawa walikuwa wengi na ndio  sababu ya show ya Diamond Kuharibika. 
 
 
0 comments :
Speak up your mind
Tell us what you're thinking... !