Home
                          
                          »
                          
                          » 
                          PHOTO;HAYA JIONEE HII;HII NDIO NDOA YA MAAJABU.MUME MMOJA WAKE WA TATU 
 
PHOTO;HAYA JIONEE HII;HII NDIO NDOA YA MAAJABU.MUME MMOJA WAKE WA TATU 
|  | 
| Anikulapo Kuti akiwa na wake zake watatu wakati wa ndoa yao. 
 FELA  Anikulapo Kuti, raia wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) ametoa  mpya kwa walimwengu kwa kufunga ndoa na wanawake watatu.
 Mtu huyo  ambaye anatumia jina la mwanamuziki  aliyevuma zamani wa Nigeria, hayati  Fela Anikulapo Kuti,  amefunga ndoa hiyo kufuatia mchungaji wa kanisa  lake nchini humo kuwaambia waumini wake kwamba wanaweza kuoa wanawake  wengi, jambo ambalo limeleta mkanganyiko mkubwa kwa waumini wa madhehebu  ya Kikristo barani Afrika.
 Ndoa hiyo ilifungwa kama kawaida, ambapo  watu hao wanne waliapa kuwa mume na wake zake, wakishuhudiwa na watu  kibao huku kiongozi aliyeifungisha ndoa hiyo akinukuu vifungu vya Biblia  ambavyo hutumiwa na Wakristo wote.
 Tukio hili limeleta mkanganyiko  mkubwa na kuwaacha watu wengi wakijiuliza mengi kuhusu madhehebu ya  Kikristo yanavyojiingiza katika matendo yasiyoendana na imani yao,  ambayo inasisitiza mke au mume kuwa na mwenza mmoja
 | 
 
 
0 comments :
Speak up your mind
Tell us what you're thinking... !