Home
                          
                          »
                          
MOVIE
                          » 
                          IRENE UWOYA ANASTAHILI PUNGEZI SOMA HAPA!
 
IRENE UWOYA ANASTAHILI PUNGEZI SOMA HAPA!
 
Pale  panapostahili pongezi ni vizuri kuitoa! nimeangalia filamu 2 jana na  leo filamu hizo ni Last Card yupo Irene Uwoya na Haji Adam(Baba Haji) na  nyingine ni HATIA yupo Hisani Muya (Tino). katika hizi filamu mbili  zote hazikuwa za kimapenzi na visa vyake ni vizuri ingawa HATIA ni nzuri  zaidi. Ila kilichonifanya niandike hapa ni kumpongeza costume and make  up artist wa HATIA maana amejitahidi sana kuwavalisha watu na kwapamba  vizuri katika mazingira ya kijijini kuku mtu wa picha nae akijitahidi  kumsaidia ili kuubeba uhalisia zaidi wa hayo maisha ya kijijini na  waigizaji wa HATIA wengi wakiwa wameuvaa uhusika vizuri hasa Tino, Bi.  Aisha na Jackson Kabirigi. Lakini katika Last Card Irene Uwoya  aliyecheza kama polisi alikuwa kichekesho katika suala la make up na  mapambo huku akishindwa kuuvaa uhusika  kama polisi. Uwoya kwenye filamu amevaa weaving la rangi inayowaka tena  la aina moja mwanzo mpaka mwisho wa filamu wakati matukio mengi ya  upelelezi yanapita lakini yupo hivyo hivyo scenes zake zote zikionekana  kama zimechukuliwa siku moja! Mbaya zaidi hilo weaving, alivyoonekana  usoni na hereni zaidi ya moja katika sikio moja alionekana kama mahabusu  badala ya kuonekana kama polisi. Wale wanaokuja kwa kesi ndio wangeitwa  polisi. Uwoya alitakiwa kuwa kawaida sana kichwani tena kwa nywele zake  halisi coz mapolisi wengi wa tanzania tunawaona wapo kawaida wakiwa  kazini hata majumbani sio masista duu kivile kama Uwoya alivyokuwa. Kama  ni nywele za bandia wengi husuka rasta na sio ma-weaving. Character ya  Uwoya ilimtaka awe polisi mchapakazi na mwenye maadili huku akiwa wa  kawaida but alivyoonekana hata aliyeongoza hiyo filamu inaonyesha hakuwa  makini na kama sikosei ni Jacob Stephen(JB). In short Uwoya alionekana  kama vile mtu ambaye alikuwa club usiku na asubuhi akakurupushwa  akiambiwa utake usitake lazima uwe polisi. Katika hii filamu hakukuwa na  make up wala costume designer kwa kumalizia tu. Picha hapo chini  haitoki kwenye filamu hiyo bali ni mfano tu
NA MWANDISHI WETU TRIM SALEEM 
 
 
0 comments :
Speak up your mind
Tell us what you're thinking... !