Jaguar kutoka Uhuru Land, Kenya ambaye kwa sasa chupa lake la Kipepeo ambalo ndio linasubiriwa kwa hamu kitaa, amegusa mioyo ya wengi baada ya kujitolea kumsomesha mwanafunzi David Owira ambaye ni msanii anayetokea katika mazingira magumu.
David alikuwa anahitaji kiasi cha shilingi za kikenya 200,000 zaidi ya shilingi milioni 3 na laki 8 za kibongo, ada ya kidato cha pili mpaka cha nne, pesa ambayo Jaguar amejitolea kusafisha yote.
Jaguar kwa sasa nyota yake imeonekana kung’ara kipesa kutokana na dili kibao ambazo amekuwa akizipiga hadi kufikia hatua ya kununua ndege yake binafsi ukiachia mbali magari ya kifahari ambayo anamiliki.
No comments:
Post a Comment