Jose  Mourinho amesema Real Madrid inaweza kuwafunga Dortmund licha ya Robert  Lewandowski (chini) kuwapa wastani wa mabao matatu yanayotakiwa  kufungwa na Madrid ili kusonga mbele.
Kocha  wa Real Madrid Mreno Mario Jose Dos Santos Ferlix Mourinho bado ana  imani kubwa kuwa kikosi chake kitabadili kipigo cha mabao 4-1  walichokipata huko Ujerumani katika mchezo wao wa marudiano dimbani  Santiago Bernabeu.
“Timu yangu mara siku zote inafanya vitu vya haki, na inaweza kushinda kwa haki katika mchezo wa leo”. Alisema Mourinho leo hii.
Kocha  huyo aliendelea kusema “Tumekubali kuwa Lewandowski alitufunga mabao  manne na hatukumfanyia hata faulo mojo. Lakini Dortmund walimfanyia  Ronaldo madhambi mara tano tangu mchezo kuanza”.
“Unawezaje  kumaliza dakika 90 bila kumfanyia madhambi mchezaji aliyekufunga mabao  manne pekee yake, ndio maana nasema timu yangu inacheza kwa haki”.  Alisisitiza Mourinho.
Leo  hii Madrid wanaingia uwanjani wakiwa na kibarua kizito cha kupindua  kipigo cha 4-1 kutoka kwa nyuki wa kaskazini mashariki mwa Ujerumani.
Mabao  yote ya Dortmund yalitiwa kambani na Robert Lewandowski lakini Mourinho  alisema timu yake haikumkaba vizuri na ndio maana Mpoland huyo  hakufanyia madhambi hata kidogo. 
Jose  Mourinho amesema Real Madrid inaweza kuwafunga Dortmund licha ya Robert  Lewandowski (chini) kuwapa wastani wa mabao matatu yanayotakiwa  kufungwa na Madrid ili kusonga mbele.
Wachezaji wa Real Madrid wakifanya mazoezi kabla ya mchezo wao wa usiku dhidi ya Dortmund uwanja wa Santiago Bernabeu 
Sergio Ramos (kushoto) na Xabi Alonso wakipasha misuli yao leo kabla ya mchezo wao wa usiku
DORTMUND
Wakati  huo huo kocha wa Borussia Dortmund Jurgen Klopp alisistiza kuwa timu  yake haitapaniki hata kidogo kupamana na Real Madrid katika uwanja wao  kwani wanajua watakuwa wanahitaji ushindi kwa nguvu zote.
Flopp aliongeza kuwa ushindi wa 4-1 nyumbani ni mkubwa sana na hadhani kama watakubali kuupoteza leo hii mbele ya Mourinho.
Alipoulizwa kama kama timu yake itashinda mchezo wa leo Flopp alisema “No, sina uhakika lakini nadhani hatuwezi”. 
Flopp  ana uhakika na alisema “Tulicheza na Bayern fainali ya kombe la  Ujerumani wakati tayari tukiwa mabingwa. Walihitaji sana ushindi  kufuatia kuwa na msimu mbaya, lakini timu yangu ilitulia na kuwapoteza  kwa wastani wa maboa 5-2.“Nadhani hata Madrid wataingia na falsafa hii ili kututoa, lakini kama hawa amini hivyo najua watambana sana”. Alisema Flopp. 
Klopp na Ilkay Gundogen wakiwa katika mkutano kabla ya mechi dimbani Bernabeu
Maandalizi: Dortmund wakifanya mazoezi kabla ya mchezo wao wa leo usiku
Wakipasha: Marco Reus (kushoto) na Mario Gotze (kulia) wakipiga jalamba
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
0 comments :
Speak up your mind
Tell us what you're thinking... !