NEY WA MITEGO AFATA NYAYO ZA DIAMOND PLATNUM CHECK NEY WA MITEGO ATUMIA MILIONI 35 KUNUNUA GARI AINA YA MARK X - HABARI ZA MPEKUZI BLOG, BOSS NGASSA, RAHATUPU BLOG AND BONGOCLANTZ
Headlines News :
Home » » NEY WA MITEGO AFATA NYAYO ZA DIAMOND PLATNUM CHECK NEY WA MITEGO ATUMIA MILIONI 35 KUNUNUA GARI AINA YA MARK X

NEY WA MITEGO AFATA NYAYO ZA DIAMOND PLATNUM CHECK NEY WA MITEGO ATUMIA MILIONI 35 KUNUNUA GARI AINA YA MARK X


Leo hii kupitia 255 ya XXL, msanii anewakilisha Manzese, Ney wa Mitego, amethibitisha kumiliki gari lenye thamani ya sh milioni 35 aina ya Mark X.
"yaa ndio gari yangu mpya hiyo, nimenunua juzi kwenye show room ya jamaa mmoja hivi anaitwa Monea, kama milioni 35 hivi, mpaka ileee mi nakuwa nayo mkononi." amesema Nay
Kwa mziki anaofanya Nay, watu wengu wamejiuliza  kama kweli mziki ndio ulimfanya kumiliki gari hilo ama kuna ishu zingine zimemuwezesha kupata ndinga hiyo.

"Mziki unachangia kwa asilimia kadhaa pia, ijapokuwa siwezi nikasema  moja kwa moja ni mziki, lakini mziki umechangia, kuna hela ya mziki pia katika hili, mi ni mfanya biashara, nafanya biashara nyingi, aaah na mziki pia ni moja kati ya biashara zangu, so mziki pamoja na biashara zingine zinafanya mi naendesha maisha yangu, na nna miliki hivi ninayomiliki" amesema Nay


Ney pia amezungumzia kuhusu picha ambayo inaonekana kwenye mtandao wa facebook, inayomuonyesha akiwa hana shati, na akiwa ameshikilia bastola..
"Aaaah,mi nahisi siko tayari kulizungumzia hilo, siko tayari tu kuongelea chochote kuhusu hiki ambacho unaniuliza sasa hivi, lakini aaah nitakapo kuwa tayari nitasema nipo tayari na nitaongea kile ambacho ntaweza kukiongea." amesema Nay


Share this article :

0 comments :

Speak up your mind

Tell us what you're thinking... !

Random Post

ARUSHA
 
Template Design by Creating Website Published by Mas Template