KILA Siku tasnia ya filamu Swahiliwood inazidi kupiga hatua na kujikuta kuna mambo yanayopaswa kuainishwa kwa wapenzi wa filamu na wadau kwa ujumla wake, tasnia ya filamu ni pana lakini kuna maeneo yanayogusa tasnia hiyo kwa ujumla wake ni waigizaji, leo tuangalia wasanii kumi bora wanaongoza kwa mauzo.
1. Marehemu Steven Kanumba pamoja na kutokuwepo hai baada ya mwaka mmoja kuondoka Duniani ameonekana kuwa ndio kinara wa mauzo hadi sasa msanii huyo ambaye amekuwa akishindana na swahiba yake Ray mauzo yake yalipanda baada ya kifo chake kuanzia mwezi wa Tano mwaka 2012.
.
.
Kanumba amerudi tena mwezi wa nne kwa kuvunja rekodi ya mauzo ya filamu baada ya filamu yake ya Love and Power kuingia sokoni filamu hiyo inampa nafasi hayati Kanumba kushika namba ya kwanza Bongo.
Nambari mbili inakwenda kwa Vincent Kigosi msanii ambaye
inasemekana kuwa toka kuanza kwake kuigiza na kuwa mtayarishaji wa filamu kazi zake hazijawahi kuyumba sokoni na kuwatia hasara wasambazaji kwani kazi zake hazidodi, Ray filamu ambazo zinampatia nafasi ya pili ni filamu ya Women of Princeple, waves of sorrow. Imemfanya azidi kupanda na kuwa juu.
Namba hii inawakutanisha wasanii wawili kwa mpigo Jacob Stephen ‘JB’ na Amri Athuman ‘King Majuto’ hawa wameweza kushiriki katika filamu nyingi lakini filamu iliyoweza kuwapa nafasi ya tatu ni Nakwenda kwa Mwanangu filamu iliuza sana.JB amekuwa ni mwigizaji wa kipekee kwa muda sasa huku King Majuto aking’ara katika vichekesho na filamu pia.
Namba hiyo pia kuna wasanii wanagongana na na kuibuka nafasi hiyo wasanii hao ni Hashim Kambi, Haji Salum ‘Mboto’ Hashim Kambi amekuwa mahiri hadi hivi karibuni alichukuliwa na kwenda kuigiza nchini Ghana, wakati Mboto ndio msanii pekee ambaye amekuwa akiigiza kama mchekeshaji pekee anayeigiza filamu kama Fall in Love, Nampenda mke wangu, Redio Presenter .
Yusuf Mlela kijana anayefanya vema katika tasnia ya filamu toka kuingia kwake katika filamu, msanii Mlela filamu zake kama Poor mind, Nifute Machozi zinampa nafasi hiyo nakuwa msanii bora namba tano.
Hao walikuwa wasanii bora wa kiume ambao wanafanya vizuri katika tasnia ya filamu toka mwezi January hadi mwezi May ukija kwa upande wa akina dada mwanadada Wema sepetu ndio nambari moja yaani Bora kwa wasanii wa kike pamoja kushiriki chache lakini ndio kinara,filamu 14 Days, It was not me, Dj Ben.
.
.
Namba mbili Inakwenda kwa mwanadada nyota Jacqueline Wolper naye kashiriki filamu nyingi lakini filamu ambayo wengi wanamuongelea ni Dreva Taxi .
Namba tatu Riyama Ali mwigizaji bingwa katika maisha ya kila aina anakuwa ni msanii mwenye kuvaa husika kwa filamu zenye huzuni, msanii ambaye ni mkongwe aliwahi kuibuka msanii bora kupitia filamu ya Fungu la Kukosa 2005/2006 Riyama msanii filamu zake ni Tabu ya kuoleana, Best wife, The Dream zimemng’arisha.
4. Jennifer Kyaka mwigizaji ambaye pia ni mtayarishaji wa filamu kwa kampuni yake ni mwigizaji ambaye anastaili kuingia na kushika nafasi ya nne filamu zinazompatia nafasi hiyo ni Rude, Pain killer.
5. Nambari hiyo inawakutanisha wasanii wawili ambao ni Aunt Ezekiel, na Ruth Suka ,Mainda , Aunty baada ya kushiriki kama I hate my birthday na nyinginezo anaibuka kwa kushiriki na filamu zake anazoshirikisha komediani filamu kama Nampenda mke wangu Radio Presenter na zingine, mainda anafanya vema na filamu ya Rude.
Hiyo ndio kumi bora katika tasnia ya filamu Swahiliwood inayofanya vizuri kwa sasa kuanzia mwaka jana hadi leo, utafiti huu kwa mujibu wa filamucentral.
0 comments :
Speak up your mind
Tell us what you're thinking... !