Habari  kamili zilizonaswa  na  waandishi  wetu  ni kwamba mwanaume aliyetajwa  kwa jina la Baba Asha alidai kumfumania rafiki yake wa karibu, Baba Tony  akiwa gesti na mkewe (jina linahifadhiwa), tayari kwa kuvunja naye amri  ya sita. 
Tukio  hilo la aibu ya milenia lilijiri katika nyumba ya kulala wageni ya  Pumzika iliyopo maeneo ya Msimbazi Center, jijini Dar ambapo mara baada  ya kumtia mikononi ‘mwizi’ wake ambaye mbali na urafiki pia ni majirani,  ndipo akamchakaza sura vibaya na kumsababishia kuvuja damu.
Habari  za kina zilidai kuwa mke wa Baba Asha alikuwa bafuni akioga, mara  ukaingia ujumbe mfupi ‘sms’ kwenye simu yake ya kiganjani, ndipo mumewe  akachukua kilongalonga hicho na kuufungua ujumbe huo.
Ilidaiwa kuwa mume alitaharuki kukutana na ujumbe uliokuwa ukimtaka mkewe kwenda Pumzika Guest House kukutana na jamaa huyo.
Iliendelea  kudaiwa kuwa Baba Asha hakuyaamini macho yake, akausoma tena ule ujumbe  na ndipo akagundua sms nyingine nyingi, vocha na fedha za mtandao  alizokuwa akitumiwa mke wake kutoka kwa Baba Tony.
Chanzo  kilidadavua kuwa baada ya kugundua mchezo mzima, Baba Asha akatulia na  kumsubiri mkewe atoke bafuni ili kuliweka sawa suala hilo.
Ilifahamika  kuwa mke aliporudi kutoka kuoga, mume hakuonesha dalili zozote,  alichokifanya ni kumwita mkewe na kumwambia kuwa achague moja,  kufungasha kilicho chake, aondoke nyumbani kwake au amwekee jamaa mtego  anaswe ili ajue mke wa mtu ni sumu.
Jibu lilikuwa rahisi kwani alikubali kuweka mtego ili amnase mbaya wake ndipo atamsamehe.
Ilifahamika  kuwa ilipita wiki moja kimyakimya kwani mara ya kwanza Baba Tony  alichezwa na machale, alipofika kwenye gesti hiyo na kumwona mtu  anayemfahamu, alimwambia yule mwanamke waahirishe.
Habari za  uhakika ni kwamba wiki iliyopita, Baba Tony aliingia kwenye kumi nane,  akajaa mzimamzima kwenye mtego wa fumanizi uliowekwa na Baba Asha na  mkewe.
Mara  baada ya kuona mwanaume mmoja (Baba Asha) akiwa na askari kwenye gesti  hiyo akihaha, king’ora kililia kwenye akili ya mwandishi wetu ambaye  hakufanya makosa, akamfuata mfumaniaji kwa nyuma hadi aliporuhusiwa  kumfuata mkewe chumbani.
Chumbani  mtiti ulikuwa mkubwa ambapo Baba Tony alikutwa kama alivyozaliwa huku  mke wa mtu akiwa bado hajavua na ndipo mtiti ukaanza.
 Katika  purukushani, Baba Asha alimpa kibano ‘mwizi’ wake hadi akamchana usoni  na kumng’oa meno ya mbele, jambo lililosababisha kutokwa na damu nyingi.
Kama hiyo  haitoshi, ili kuthibitisha kuwa mke wa mtu ni sumu, Baba Asha alimchoma  jamaa huyo bisibisi kwenye makalio hadi askari alipoingilia kati na  kumchukua mtuhumiwa kisha akamtoa nje.
Wakiwa  nje ya gesti hiyo, Baba Tony aliomba kujisafisha damu na baada ya hapo  alipigwa pingu tayari kwa kupelekwa Kituo cha Polisi, Pangani, Ilala...
SOURCE ; GLOBAL PUBLISHERS
 
 



 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
0 comments :
Speak up your mind
Tell us what you're thinking... !