MWENYEKITI wa 
Kamati ya Mashindano ya Miss Tanzania, Hashimu Lundenga Jumamosi 
iliyopita alimtimua mshiriki wa shindano la Redd’s Miss Morogoro 2013, 
Saphina Chumba (20) jukwaani wakati shindano hilo lilipokuwa 
likiendelea.
Tukio hilo lilitokea Jumamosi iliyopita katika Ukumbi 
wa Hoteli ya Kitalii ya Nashera mjini hapa wakati mrembo huyo alipokuwa 
akiwania kuvaa taji la mkoa huo.
Kisa cha mrembo huyo aliyevalia namba 5 kutimuliwa ni kukiuka maadili na kanuni za mashindano hayo kwa kuvaa nusu utupu mbele ya mgeni rasmi ambaye alikuwa Mbunge wa Kilosa, Mustapha Mkulo na mbele ya Kamati nzima ya Miss Tanzania.

Baada ya kuona jinsi alivyovaa, Lundenga na 
kamati yake walikubaliana kumtimua mshiriki huyo kwa kumwita Jaji Mkuu 
wa shindano, Alex Niktasi na kumtaka amuondoe haraka.
Mbali na 
Chumba, pia jaji alimtimu mrembo mwingine aliyevalia namba 8, Neema Joel
 (20) kutokana na kushiriki shindano  hilo mara mbili mwaka huu, 
inadaiwa mara ya kwanza alishiriki mkoani Arusha. 
Lundenga 
alipohojiwa na mwandishi wetu alisema kamati yake inataka kuendeleza 
nidhamu tangu ngazi ya chini, hivyo hawawezi kuruhusu utovu wa nidhamu.
 
0 comments :
Speak up your mind
Tell us what you're thinking... !