MISS Tanzania 2006 ambaye pia ni mcheza filamu mkali Bongo, Wema Isaac  Sepetu, hivi karibuni alikumbwa na kizaazaa cha kutaka kutekwa na watu  wasiojulikana wakimtuhumu kuwatukana kupitia Facebook.
Mrembo  Wema Isaac Sepetu.
Akizungumza na Amani jijini Dar juzi, Wema alisema tukio hilo  lilimtokea Kijitonyama, Dar wakati akitoka kwenye mishemishe zake  kuelekea nyumbani kwake.
Alisema alipofika maeneo hayo, gari asilolijua lilimpita na kwenda kusimama mbele yake kisha wakashuka watu asiowajua na kuanza kumuuliza ni kwa nini anawatukana katika mtandao wa kijamii wa Facebook.
“Nilivyosikia wanasema Facebook, roho yangu ikatulia maana najua kuna watu kama 37 wanaotumia jina langu na picha zangu kwenye Facebook, nilishuka kweye gari na kuanza kuwaelewesha kuhusu hilo, bahati nzuri walinielewa,” alisema Wema.

0 comments :
Speak up your mind
Tell us what you're thinking... !