 NEW YORK, Marekani
VIDEO iliyoonyweshwa mwishoni mwa wiki katika mitandao mbalimbali ya kijamii, ambayo ilielezea madhara ya taratibu anayoyapata mwanamke aliyeongeza ukubwa wa makalio, kwa dawa za silkoni imewashtua wanawake wengi waliowahi kutumia aina yoyote ya madawa hayo.

Taarifa hiyo ilieleza kuwa madawa hayo badala ya  kumfanya mwanamke awe laini, video hiyo inaelezea namna ukuaji wa haraka  wa makalio pamoja na kuathirika huku yakiachwa katika sura mbaya sehemu  za nyuma (chini) baada ya muda mfupi.
Imebainika kuwa pamoja na dawa za kuongeza ukubwa  wa makalio ya akina dada kupendwa, dawa hizo pia zina madhara kwa afya  ya binadamu.
Wataalamu wa mambo wanadai kwamba pamoja na  kuongeza ukubwa wa makalio pia dawa huleta matatizo ya kuvimba kwa ngozi  ya makalio katika mpangilio usio sahihi.
Dawa hizo pia zimetajwa kuwa husababisha kwa uwepo mkubwa wa ugonjwa wa saratani.
Video hiyo ya sekunde 20, inamwonyesha mwanamke aliyeongeza makalio yake kwa dawa za silicone akionyesha namna alivyoathirika kutokana na matumizi ya madawa hayo huku akisema : "Hivi ndivyo nilivyoongeza ukubwa wa makalio yangu".

Anaongeza: "Sidhani kama ni sahihi kufanya hivi.  Nadhani kuna ulazima wa kuyaondoa haya makalio yangu yote kwa sasa."  alisikika akisema.
Mpaka kufikia jana video hiyo ambayo pia iliwekwa  katika mtandao wa kijamii wa Facebook tayari ulikuwa umependezwa na watu  278,000 wanaotembelea huku ikiwa imehamishwa na watu zaidi ya 430,000  wakipeleka katika kurasa zao.
Mtumiaji mmoja wa mtandao huo kutoka nchini  Marekani Donna Wright-Levy, alichangia akisema: "Mimi hupendelea kwenda  maeneo kadhaa ambako hutengenezwa shepu yangu kwa madawa haya sasa nina  ulazima wa kwenda kupima saratani".
Ni vigumu kuthibitisha mwanamke huyu alitumia  kliniki gani wakati alipofanyiwa uongezwaji wa ukubwa wa makalio yake  miaka miwili iliyopita.
Lakini mmoja wa madaktari kutoka kliniki ya  upasuaji ya BAAPS Aurora nchini Uingereza Adrian Richards, ambaye pia ni  mshauri wa upasuaji anaamini kuwa mwanamke huyo alifanyiwa marekebisho  ya makalio yake kwa dawa za silicone.
Alisema tatizo hutokea wakati nyama ya makalio  inaposhindwa kuulinda vema mwili na kuwa imara katika nyama na mifupa na  hivyo madhara huanza kutokea juu ya ngozi na kusambaa mpaka ndani ya  nyama na baadaye mfupa.
Ni matatizo ambayo ni ya kawaida kumfika mtumiaji  ya dawa za kuongeza ukubwa wa maumbile iwe ni matiti ay makalio. Ni  lazima itokee baada ya muda maana kama kitu kilipulizwa na upepo ina  maana wakati wake ukiisha kitarudi kama awali.
                               "Huyu mwanamke aliyaongeza makalio yake kwa nyuma  na kwa juu zaidi hivyo tayari madhara yake yamekuwa ni makubwa kwa maana  hakufanya upasuaji bali alitumia njia za mkato za silicone, " alisema  Richards.
 
0 comments :
Speak up your mind
Tell us what you're thinking... !