



kushuhudia onyesho la kwanza la Tamthilia mpya iitwayo Siri  ya Mtungi. Tamthilia mpya hii ya
 kusisimua itatangazwa kila wiki siku ya  Jumampili saa 3:30 usiku kwa njia ya ITV na kurudiwa saa 3:30 usiku  jumaatanu ifuatayo kwa njia ya EATV.
Tamthilia  hii mypa imetekelezwa na JHU-CCP (John Hopkins Bloomberg School of  Public 
Health Center for Communication Programs); kwa msaada wa Watu wa  Marekani (USAID – United States Agency for International Development) na  PEPFAR (US President's Emergency
 Fund for AIDS Relief). Ikiwa  imetayarishwa na MFDI (Media for Development International) na
 inwaleta  pamoja Wasanii bora wa Tanzania, waandishi, wana mitindo  nguo,wakurugenzi wa 
sanaa, waigizaji na watendaji wa filamu kwenye  mafanikio makubwa ya ukuaji wa tasnia ya filamu na televisheni Tanzania.  Pia tamthilia hii ni kati ya juhudi za programu ya awali ya TCCP  (Tanzania Communication Capacity Project).
Katika  maonyesho hayo, huko Msasani, wadau walikaribishwa na kupata fursah ya  kuonana na waundaji, waandishi, waigizanji na watekelezaji wengine wa  tamthilia hiyo. Pia walipata fursah ya kuhudhuria studio hiyo na kuona  waigizaji wakiigiza kipande kidogo cha tamthilia hiyo pale pale studio  akiwemo muigizaji mahiri hapa mjini wa Monalisa!
Kwa habari zaidi kuhusu Siri ya Mtungi jiunge na kurasa wao wa 
Facebook (www.facebook.com/SiriyaMtungi) au fuatilia mtiriko wa uhondo huko Twitter kwa kujiunga na @SiriyaMtungi (http://www.twitter.com/SiriyaMtungi). Pia chukuwa fursah kupitia tovuti ya tamthilia (www.siriyamtungi.com  
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
0 comments :
Speak up your mind
Tell us what you're thinking... !