Gari  walilopata nalo ajali Salma Salmin ‘Sandra’, Nuru Nassoro ‘Nora’ na Jasmini Nyaku.
Kwa mujibu wa chanzo makini, wasanii hao walikuwa ndani ya gari aina  ya Toyota Fun Cargo lenye namba za usajili T 402 CDU ndipo wakapatwa na  msala huo maeneo ya ‘round about’ ya Mlimani City, Dar ambapo gari  liliacha njia na kupinduka bila sababu ya msingi.
“Gari halikuwa spidi kiivyo lakini ghafla tukashangaa kuona linagonga  ukingo wa barabara na kupinduka ndipo tulipoanza kuwapa msaada na  kuwapeleka hospitali,” kilisema chanzo hicho.
 Salma Salmin ‘Sandra’.
Nora alipopatikana alifunguka:
“Ilikuwa ghafla tu, tulikuwa mimi, Nyaku, Sandra na mumewe ndani ya gari. Dereva alikuwa Jasmini tukashangaa gari linaacha njia na kupinduka bila sababu yoyote.
“Nimepata majeraha madogomadogo mkononi, Sandra ndiyo aliumia zaidi  kichwani, hivyo tulilazimika kumpeleka Hspitali Kwamama Ngoma, Mwenge  kisha tukaambiwa tumhamishie Muhimbili alikolazwa hadi sasa hivi.”
Nuru Nassoro ‘Nora’.
CREDIT KWA GLOBAL PUBLISHERS 
 
 



 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
0 comments :
Speak up your mind
Tell us what you're thinking... !