 
  Q  Chilla amesema kuingia kwake kwenye matumizi ya madawa ya kulevya  ilisababishwa na baadhi ya watu kuchangia kumrudisha chini na kujikuta  yuko peke yake katika mitihani aliyokuwa akipitia. 
Huku akikataa kuwataja kwa majina alisema watu hao walihakikisha kila  anachokifanya hakifanikiwi na kujikuta katika wakati mgumu.  Qchilla  amesema alishindwa kujua amemkosea nani au nani amuombe msamaha.
Hata hivyo anasema anawashukuru watu wake karibu waliokuwa  wakisikitishwa na hali aliyokuwa nayo na kuamua kumshauri aache kutumia  madawa hayo.ujanatz blog
Alipoulizwa anawashauri vipi wasanii ambao wametumbukia kwenye  matumizi hayo alisema njia pekee ni kukubali kuwa wana tatizo na  kuishika dini.
Pia aliipongeza hatua ya rais Kikwete kumsaidia Ray C ambaye pia  alikuwa aliingia katika wimbi hilo akitolea mfano wa rais Nelson Mandela  aliejaribu kumsaidia mwanamuziki Brenda Fassie na Rais Obama  aliemsaidia marehemu Whitney Houston na kusisitiza wasanii wote ambao ni  waathirika wa madawa ya kulevya kujitokeza ili wasaidiwe na jamii.
QChilla amesema kwa sasa anafanya muziki akilenga soko la kimatafifa  zaidi akiwatolea mfano PSquare na kusema tatizo la wanamuziki wengi  kuishia kusikika nchini tu ni kujiwekea mipaka na kulenga soko la ndani  tu na kumalizia hana mpango wa kutoa album badala yake ataendelea kutoa  nyimbo kali.
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
0 comments :
Speak up your mind
Tell us what you're thinking... !