Wakati  miamba ya soka la Hispani, Real Madrid wakikabiliwa na kibarua kizito  hapo kesho kuhitaji ushindi wa mabao 3-0 mbele ya nyuki wa kaskazini  mashariki mwa Ujerumani, Borussia Dortmund, katika mchezo wa fainali ya  pili ya Ligi ya mabingwa barani ulaya, mshambuliaji wa zamani wa Man  City, sasa akikipiga AC Milani na timu ya taifa ya Italia “The Azzuri”,  Mtukutu Supa Mario Balotell ametoa kali baada ya kumtumia mpenzi wake  Mbelgiji Fanny Neguesha kuwakebehi Real Madrid kuelekea kipute cha  kesho.
Balotell  amesema ana imani kubwa Dortmund watafuzu hatua ya fainali na kama Real  Madrid watawatoa katika mchezo wa kesho na kucheza fainali Wembley  mwaka huu basi atawapa idhini ya kulala na mpenzi wake kwa usiku mzima.
Mgazeti  ya Hispania ya AS NA Marca yamemkariri nyota huyo wa AC Milan akisema  “Kama Real Madrid watafuzu fainali ya UEFA mwaka huu baada ya kufungwa  4-1, nitawaachia mpenzi wangu alale nao”.
Akitabasamu:  Mario Balotelli  akishangilia baada ya kuzamisha gozi kambani kwa njia  ya mkwaju wa penato dhidi ya Catania usiku wa jana.
Mpenzi  wa Balottell  Fanny Neguesha ambaye amechora Tattoo ikieleza hisiza  zake za kimapenzi kwa Balotell, endapo Madrid watafuzu mtoto mzuri yupo  kwa ajili yao leo
 Balotelli na Neguesha mahusiano yao yamejengeka zaidi baada ya nyota huyo kuihama City na kuhamia AC Milani.
Dortmund  waliwatandika kipigo cha Mbwa mwizi Real Madrid huku Robert Lewandowski  akipiga goli zote nne.Manchester United na Bayern Munich  zote  zinaitaka saini ya Lewandowski.Cristiano Ronaldo ambaye alufunga bao  moja la kufutia machozi wikiendi iliyopita alikosa mchezo wa timu yake  dhidi ya Atletico Madrid kufuatia kuwa majeruhi, lakini leo amefanya  mazoezi na kocha Mourinho amefurahishwa na kurejea kwa nyota wake.
Robert Lewandowski  atafanya nini Santiago Berbeu usiku wa kesho
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
0 comments :
Speak up your mind
Tell us what you're thinking... !