Mimi ni mdada wa miaka 27 na nina watoto wawili kwa sasa  nimeolewa na mkaka mwenye miaka 32.
Kwa kweli mume wangu ni  kijana handsome. Katika maisha yangu ya  usichana mpaka kuolewa nimekuwa na mahusiano na wanaume takribani 4  kabla ya mume wangu.
Wanaume hao wote kwakweli walikuwa nao  wazuri  na kati yao wawili walikuwa waume za watu na  walikuwa na maumbile yakunitosha.... 
Pamoja na maumbile  yao,sikuwahi kufika kileleni japokuwa  walikuwa wanapumzi ndefu yaani walikuwa wanaweza kuplay for about  1 hour . Tena kama tutalala pamoja usiku huo  walikuwa wanaweza hata 4-5.
Nilipompata mume wangu nilimpenda toka  rohoni na baada ya mhusiano ya miaka miwili tulioana,tatizo ambalo lipo  kwenye ndoa yangu na nililiona toka mwanzo ni kwamba mume wangu hana  pumzi kitandani japokuwa ndio mwanaume pekee anayenifikisha kileleni .
Yaani  mume wangu yeye ni 3 minutes tu amemaliza  na baada ya muda  anakoroma, hatuwezi kufanya hata mara  mbili kwa usiku hata nikimchezea anashindwa kusimama labda afanye kimoja asubuhi kingine usiku.
Na  ili nikojoe kuna staili lazima niziapply mimi mwenyewe niwe najigusa  kwake maana yeye tukifanya anashindwa kujizuia mara moja anakojoa.
Nisaidieni wapendwa nifanyaje maana  bado  nampenda  mume  wangu."
---------------
Jibu la Dyna: 
Shukurani sana kwa ushirikiano, hongera kwa kufanikiwa kufika kileleni  kwani sio wanawake wote hufika hapo.  Sidhani kuwa ni kweli kuwa mumeo  anakojoa ndani ya dakika 3 na wakati huohuo wewe unafika kileleni. 
Unapokuwa  kwenye uhusiano wa kudumu au ndoa hupaswi kabisa-kabisa kurudisha  mawazo yako nyuma na kuanza kufananisha utendaji wa wanaume uliokuwa nao  na mpenzi wako wa sasa/mumeo. Jifunze kukubali jinsi mumeo alivyo na  ridhika na uwezo wake aliojaaliwa na Mungu.
Ndio maana kabla ya  uchumba kutangazwa kule kwetu huwa kuna swali unaulizwa na  mama au bibi au shangazi
- "je una uhakika kuwa unataka kuolewa na huyu bwana? 
-je uko radhi kuishi nae hata kama siku moja utagundua kasoro zake?  (kasoro hapa wanamaanisha kushindwa kufanya tendo). 
Hivyo basi  unapofunga ndao na mtu na kugundua kuwa uwezo wake kitandani  umebadilika ghafla kutokana na umri au mataizo mengine ya kiafya,  unatakiwa kukubali tatizo na kumpa ushirikiano ili kuepusha matatizo.
Kilele na mwanamke:
Mwanamke  anafika kileleni kuanzia Dk 10 mpaka dk 45 tangu tendo lianze na  pengine inaweza kuchukua muda mrefu zaidi, hivyo basi kama unafanikiwa  kufika kileleni ni wazi kuwa mumeo anauwezo wa kwenda mwendo wa angalau  Dk15-20 sio dakika  3  kama  ulivyosema!
Napenda  utambue kuwa uwezo wa tendo kwa wanawaume unatofautiana kama ilivyo  kwa baadhi ya wanawake, suala muhimu ni upendo mlionao (mnapendana) na  yeye anauuwezo wa kulifanya tendo mpaka wote mnafikia  mshindo nakuridhika.
Mawasiliano wakati wa Tendo:
Suala  lingine hapa ni kutojua namna ya kucheza na wewe au mwili wako, kama  unapenda kuchezewa zaidi kabla ya tendo la ndoa ni wajibu wako kuliweka  hilo wazi na kumuelekeza mumeo wapi pa kushika, usitegemee yeye  afanye hivyo kwani hajui nini unachokitaka au kukipenda. Ili ufurahie  tendo na lifanywe your way unatakiwa kuwasiliana na mumeo wakati tendo  linaendelea....
Kama  nilivyosema hapo awali sio wanaume wote wanauwezo wa kufanya  mapenzi  unaofanana, hivyo basi kama yeye anamudu asubuhi na jioni au asubuhi  mchana na jioni (weekends) then kubali utaratibu huo kuliko kulazimisha  afanye ulivyozoea wewe mara tatu katika saa moja.....ni ngumu kwa baadhi  ya wanaume hasa wenye umri wa miaka 35 na zaidi.
Ni  matumaini yangu utafanyia kazi ushauri kutoka kwa wachangiaji wengine  na kuongezea maelezo ya hapo juu  ili kuishi maisha mazuri na yenye  amani kwa faida yako, mumeo na watoto wenu
 
 


 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
0 comments :
Speak up your mind
Tell us what you're thinking... !