Wakati mwingine mtu unakuwa umechoka na  usingependa kupoteza muda jikoni, so mlo wa chapchap unakuwa ni wazo  zuri, Mlo huu ni rahisi kuuanda na hata haikuchukui zaidi ya dakika  ishirini chakula kinakuwa tayari mezani.
Mahitaji
Salmon fillet 2Potatao wedge kiasi
Lettice kiasi
Cherry tomato
Limao 1
SwaumChumvi
Olive oil
Matayarisho
Mmarinate  samaki na chumvi, swaum na nusu ya limao kisha muweke pembeni, baada ya  hapo washa oven kisha tia potato wedge zikisha karibia kuiva anza  kumpika samaki, tia mafuta kidogo sana kama kijiko kimoja cha chai hivi  katika frypan isiyoshika chini yakisha pata moto kiasi muweke samaki  wako (upande wenye ngozi chini kwanza) Mpike mpaka uone rangi ya kahawia  kwa chini kisha mgeuze upande wa pili, uku samaki wako akiwa anaendelea  kuiva, tayarisha salad yako kwa kusafisha lettice na nyanya kisha  zichanganye pamoja kisha tengeneza salad dressing pembeni , kamua limao  kisha tia olive oil na chumvi kidogo, Baada ya hapo samaki na potato  wedge vitakuwa vimeiva, andaa mlo wako na utakuwa tayari kwa kuliwa. 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
0 comments :
Speak up your mind
Tell us what you're thinking... !