Rehema Chalamila ‘Ray C’.
Baadhi ya watu walianza kuamini uzushi huo na kujiuliza kulikoni katika burudani Bongo kuwapoteza mastaa wao mfululizo.
“Juzi tu Mlopelo, halafu John Maganga, jana (Jumatatu) Sharo Milionea. Leo tena Ray C, kuna nini kwa mastaa wetu?” alihoji mmoja wa watu waliotumiwa ujumbe huo huku akishika kichwa kuonesha hali ya majonzi.
Mama mzazi wa Ray C, Margaret Mtweve.
Hata hivyo, hadi kufikia saa 4 usiku, mama mzazi wa Ray C, Margaret Mtweve alijitokeza hadharani kupitia Radio Clouds FM na kukanusha vikali taarifa hizo huku akisema:“Mwanangu ni mzima, tena anaendelea vizuri kwa sasa. Hao wanaoneza uzushi huo washindwe kwa jina la Yesu.”
Awali, mchana wa siku
hiyo, zilienea tetesi eti msanii nyota wa sinema Bongo, Juma Sadiki Kilowoko ‘Sajuki’ naye amefariki dunia wakari si kweli.
Ray C.
Watu waliozungumza na gazeti hili jana walionesha wasiwasi wao mkubwa juu ya ufahamu wa baadhi ya Watanzania ambao wamekuwa na tabia ya kueneza uvumi mara kwa mara kwamba mtu f’lani, hasa maarufu amefariki dunia.“Nahisi kuna Watanzania si wazima vichwani kwani sasa imekuwa fasheni. Mtu anaamua tu, anaandika ujumbe kwenye simu kwamba staa f’lani amefariki dunia wakati si kweli,” alisema Hamad Hussein, mkazi wa Magomeni-Kagera, Dar.
0 comments :
Speak up your mind
Tell us what you're thinking... !